Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sheikh Ali al-Khatib, Makamu wa Rais wa Baraza Kuu la Kiislamu la Kishia la Lebanon, baada ya kukamilisha safari yake katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amerejea mjini Beirut.
Sheikh al-Khatib, akiwa katika ukumbi wa wageni mashuhuri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Beirut, alisema: Tulijivunia kusafiri hadi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kushiriki katika Mkutano wa kukurubisha Madhehebu ya Kiislamu, hii ilikuwa fursa ya kubadilishana mawazo na viongozi wa wajumbe wa mataifa na baadhi ya maafisa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusu ulazima wa uratibu kati ya wanazuoni wa Kiislamu na nchi za Kiislamu, na kutoa mapendekezo katika sekta hii.
Akaongeza kusema: Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu atujalie tawfiki katika kufanikisha lengo hili, jambo ambalo ni la dharura hasa baada ya mabadiliko ya hivi karibuni yaliyotokana na mashambulizi ya Israel dhidi ya Qatar.
Makamu wa Rais wa Baraza Kuu la Kiislamu la Kishia la Lebanon aliendelea kusema: Baada ya mauaji ya halaiki yaliyofanywa na adui wa Kizayuni huko Ghaza na mashambulizi dhidi ya Lebanon, uratibu huu kati ya nchi za Kiarabu na Kiislamu, na pia mkutano unaotarajiwa kufanyika kesho huko Doha, unapaswa kuwa fursa ya kuimarisha mahusiano haya na kubuni mkakati wa Kiarabu-Kiislamu wa kusimama imara dhidi ya kiumbe huyu katili asiye na kifungo wa Kizayuni, ambaye sasa hana kizuizi chochote cha kushambulia nchi yoyote ya Kiarabu.
Sheikh al-Khatib aliendelea kusema: Katika uwanja wa Lebanon, pia siamini kwamba kuna ushahidi mkubwa zaidi ya ule uliojitokeza katika shambulio dhidi ya Qatar, hususan baada ya kuwepo ushahidi mwingi uliothibitisha kwamba adui huyu hatilii maanani sheria wala makubaliano ya kimataifa, na anaendelea kutumia nguvu kuuvamia ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu, hasa Lebanon.
Alisisitiza ulazima wa kuhifadhi uhusiano wa Walebanon, mshikamano wa Walebanon, kutoka katika hali ya migawanyiko ya kisiasa, na kudumisha umoja wa jamii za Kiarabu na Kiislamu katika kila nchi; na akasema kuwa hakupaswi kuwa na tatizo la ndani, bali jitihada zote zinapaswa kuelekezwa katika umoja na msimamo mmoja mbele ya adui wa “Kizayuni” kwa ajili ya kulinda na kutetea ulimwengu wa Kiarabu na mataifa ya Kiislamu na kukomesha mauaji ya halaiki yanayoendelea Ghaza.
Makamu wa Rais wa Baraza Kuu la Kiislamu la Kishia alieleza matumaini yake kwamba mkutano wa Doha utazaa maamuzi ya hatima, na kwamba sisi tusibaki tena, kama ilivyokuwa awali, tukiwa na maneno matupu bila ya matokeo ya kivitendo.
Mwisho, alionyesha pia matumaini kuwa yatakayotokea Doha yatakuwa msukumo wa kuchukua hatua za kivitendo na za kuzuia ili kukabiliana na uvamizi huu wa kinyama na usio na huruma.
Maoni yako